Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya akitoa tamko kwa waandishi wa habari jana jijini Arusha,ambapo amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake
Katibu hamasa Mkoa wa Arusha Lucas Msomi akisisitiza jambo katika kikao na waandishi wa habari
Baraza la vijana mkoa wa Arusha la chama cha mapinduzi uvccm limetangaza kumvua ukamanda wa vijana wilaya ya Arumeru bw,Mathias Manga kutokana na kukiujumu chama kwa muda mrefu hali ambayo imekuwa ikididimiza jitihada za kurejesha imani ya chama hicho.
Bw,Manga ambaye ni mafanyabiashara maarufu wa madini Mkoani Arusha amekuwa akituhumiwa kwa muda mrefu kuwa namhausiano ya karibu ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa na kusahau kufanya majukumu ya kichama ambayo yamempa uongozi wa Ukamanda wa vijana wilaya.
Akitoa maelezo ya tamko hilo mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Lengay Ole Sabaya amemtaja Mathias Manga na washirika wake kuwa ni tatizo kubwa ndani ya chama na kwamba kama akiendelea kuwepo ni Dhahiri kuwa anaweza kukisambaratisha chama hicho kutokana na kugawa makundi kwa vijana wa chama hicho kutokana na fedha zake.
Aliongeza kuwa kutokana na kumvua ukamanda kamanda huyo UVCCM Mkoani hapa haitakuwa tayari kushiriki kikao chochote cha kamati ya siasa ambapo Manga atashiriki kama mjumbe katika kikao hicho.
,,Sitashiriki kwa namna yeyote na vijana wangu kwenye kikao cha kamati ya siasa Mkoa ama kikao kingine ambacho kitanikutanisha na Mathias Manga na nawataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuona kama ni halali kwa huyu aliyeitwa kamanda wa vijana kuendelea kushikilia kadi yao,,Alisema Ole Sabaya
Akitoa onyo kwa makamanda wilaya ya Arusha mjini,Longido na Monduli kujipima na kujitathimini kabla ya kufikia uamuzi kama bado wanafaa kuendelea na hadhi ya ukamanda wa wilaya ama laa,na wakijiona hawatoshi tunawashauri wakae pembeni mapema kabla ya kutumbuliwa jipu.
Baraza linakiomba chama cha Mapinduzi kupitia tathini ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana wale wote walioshiriki kukihujumu chama kuanzia ngazi ya matawi,kata,wilaya na Mkoa washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu za kimaadili kabla ya uchaguzi wa chama 2017 vinginevyo wakiachwa watashiriki tena kufanya uhasi dhidi ya chama sanjari na kupandikiza mamluki.
Hata hivyo mwenyekiti huyo ametengua uteuzi wa wajumbe watano wa baraza katika nafasi za kuteuliwa ilidumu toka mwaka 2012 na kuunda kamati mpya chini ya mwenyekiti Lengai Ole Sabaya huku akiwataka viongozi wa chama hicho kumuunga mkono Rais JohnPombe Magufuli kwa jitihada zake za kupeperusha bendera ya chama na kufanya kazi kwa uadilifu na kubeba kauli ya HAPA KAZI TU.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakikaribishwa ukumbini na kupewa kinywaji cha K -Vant ambao walikua wadhamini wa shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakifurahia kinywaji cha K-Vant.
Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima akakitambulishwa ukumbi kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mkoa wa Arusha. Katikati ni Mkurugenzi wa Mwandago Investment, Chris Mwandago ambaye ni muandaji mashindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na kulia ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akizungumza jambo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akikata utepe kuzindua mashindano hayo jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (kulia), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia) na Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima.
Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Wadau wa tasnia ya urembo wakifurahia jambo.
Baada ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa shirikisho la waajiri la jumuiya ya Afrika Mashariki(EAEO),Rosemary Ssenabulya akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivikaribuni kuhusu mafanikio na changamoto za shirikisho hilo,kushoto kwake ni katibu wa shirikisho hilo,Agrey Mlinuka na kulia kwake ni mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la waajiri nchini Kenya,Jacqueline Mugo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rishwa (TAKUKURU) imewafikisha Mahakamani hii leo Wabunge watatu kwa tuhuma za kupokea rushwa iliyotolewa katika kamati zao. Wabunge hao pichani kutoka kulia ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Mvomero, Sadiq Ahmed Murad na Mbunge wa Mwibara , Kangi Lugola.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayoshirikiana na Serikali ya Tanzania kutoa huduma katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyoko wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ibungho, Anatory Nsamizanala(wa kwanza kushoto), mara baada ya kufika katika shule hiyo inayotoa elimu ya awali katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Gerald Guninita.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri (wa pili kulia), kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Mabamba kilichopo wilayani Kibondo,mkoani Kigoma.Kituo hicho cha Polisi kinajengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR). Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Exavery Christopher (aliyevaa kofia nyeupe), akitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wa kwanza kushoto), wakati akijibu maswali aliyoulizwa na Naibu Waziri muda mfupi baada ya kuwasili katika kituo cha Uhamiaji cha Mabamba tayari kwa kusajiliwa kabla ya kupelekwa kambini.Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri. Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ikiwemo kutembelea kambi za wakimbizi zilizopo ndani ya mkoa wa Kigoma.Ziara iliofanyika tarehe 30/3/2016.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Lwekatare akitoa taarifa ya mradi wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Msajili Masaidizi wa Hazina Jones Mwalemba akitoa ufafanuzi namna ofisi yake inavyochangia katika kukamilisha mradi wa mabasi yaendayo haraka wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………..
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa ifikapo Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi 31, 2016 kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili kuhakikisha wanatoa huduma ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri mradi huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema iwezekanavyo” alisema Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi sasa mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za mradi huo na kuwahimiza wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya majaribio angalau yafike 15 ili madereva wazoee barabara kabla ya mradi kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha mradi huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo haraka wawe na utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi walizojipangia na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia taarifa kila baada ya siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa wa kazi wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi huo imekamilika na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo waitunze miundombinu hiyo ikiwemo barabara na vifaa vitakavyokuwa vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya DART ni kulihujumu taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao ili mradi uwe wa tija kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau wa mradi wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake Selemani Jaffo pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi kupitia eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140 ambayo yanatarajiwa kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es Salaam.
Kikao cha Waziri Simbachawene kilihuwahusisha wadau wa mradi huo ambao ni DART, TANROAD, Msajili wa Hazina, Kampuni ya Simon Group, SUMARTA, Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na Jeshi la Polisi.
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakikata utepe wakati akizindua ripoti ya utafiti wa utoaji wa mimba usiosalama uliofanyika nchi nzima ambao umefanyika kwenye ukumbi wa JNICC leo jijini Dar es salaam leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU -FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili wakionyesha utafiti huo mara baada ya kuuzindua rasmi.
Dr. Neema Lusikamayki Mkurugenzi wa Huduma Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akisoma hotuba yake kabla ya kuzindua utafiti huo katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.
Profesa PS Muganyizi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili akiungumza na waandishi wa habari kabla ya uzinduzi huo katikati ni Sarah Keogh kutoka taasisi ya Guttmacher ya nchini Marekani na kulia ni Andrea B. Pembe Kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya Muhimbili.
Baadhi ya wataalamu na waandishi wa habari mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wataalamu namaofisa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Utafiti mpya Watoa Makadirio ya Kwanza Kitaifa ya Matukio ya Utoaji Mimba Nchini
Katika utafiti wakilishi wa kwanza kitaifa kuhusu matukio ya utoaji mimba na huduma baada ya kuharibika kwa mimba nchini Tanzania, watafiti waligundua kwamba utoaji mimba kwa siri hutokea mara nyingi na huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye vifo na kuumia kwa wajawazito. Utafiti huo, uliofanywa na watafiti kutoka taasisi ya Guttmacher iliyoko Marekani, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili zilizoko hapa Tanzania, waligundua ya kwamba makadirio ya mimba 405,000 zilitolewa nchini ndani ya mwaka 2013, nyingi zikitolewa kwa taratibu ambazo si salama na kuhatarisha maisha ya wanawake. Kutokana na mchanganyiko wa sheria tata na yenye vizuizi vingi ya utoaji mimba ya Tanzania, wanawake hutafuta huduma za utoaji mimba zinazofanyika kisiri na ambazo si salama.
Watafiti hao, ambao walifanya utafiti kwenye vituo vya afya, miongoni mwa wataalamu wa afya na kufanya mapitio ya taarifa za idadi ya watu na uzazi, wamekadiria kwamba wanawake 66,600 walipewa huduma baada ya kuharibika kwa mimba kwenye vituo vya afya kutokana na matatizo yaliyotokana na utoaji mimba usio salama ndani ya mwaka 2013. Hata hivyo, karibu wanawake 100,000 ambao walipata matatizo hawakupata matibabu ambayo waliyahitaji. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo yao yatasaidia kutaarifu juhudi zinazoendelea nchini Tanzania kupunguza uwiano wa vifo vya wajawazito, ambao umebaki kuwa miongoni mwa iliyo juu zaidi duniani.
“Kwa kutambua kuwa utoaji mimba usiokuwa salama ni chanzo kikuu cha vifo vya wajawazito, Serikali ya Tanzania imepanua wigo wa upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba katika muongo mmoja uliopita, lakini mapungufu makubwa bado yapo na wanawake wengi hawapati huduma wanazohitaji,” alisema Sarah C. Keogh, mtafiti mwanasayansi mwandamizi wa taasisi ya Guttmacher na mwandishi kiongozi wa utafiti huo. “Utafiti huu unabainisha mapungufu hayo na kusaidia kuunda mikakati kuhakikisha kuwa kila mwanamke wa Kitanzania anayehitaji anaweza kupata huduma baada ya kuharibika kwa mimba inayoweza kuokoa uhai.”
Kiwango cha kitaifa cha utoaji mimba nchini Tanzania—36 kwa kila wanawake 1,000 walio kwenye umri wa uzazi—kinafanana na viwango vya nchi nyingine za Afrika Mashariki. Hata hivyo, ndani ya Tanzania viwango vya utoaji mimba vinatofautiana kwa ukanda. Viwango vya juu ya utoaji mimba hupatikana katika Kanda ya Ziwa (51 kwa kila wanawake 1,000) na Nyanda za Juu Kusini (47 kwa kila wanawake 1,000), na kiwango cha chini hupatikana Zanzibar (11 kwa kila wanawake 1,000). Viwango hivi tofauti vya utoaji mimba huhusishwa kimsingi na utofauti katika viwango vya matumizi ya njia za uzazi wa mpango na mimba zisizotarajiwa, na uwezekano wa wanawake kuamua kutoa mimba katika tukio la kupata mimba zisizotarajiwa.
“Mbali na huduma baada ya kuharibika kwa mimba, wanawake wa Kitanzania wanahitaji upatikanaji bora na kamilifu wa huduma mbalimbali za njia za uzazi wa mpango na ushauri nasaha kuhusu uzazi wa mpango ili waweze kufanya maamuzi sahihi,” alisema Godfather Kimaro, mwanasayansi mtafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania, ambaye alifanya kazi kwenye utafiti. “Ndani ya mwaka 2013, wanawake wa Kitanzania walipata mimba zisizotarajiwa zaidi ya milioni moja, ambazo kati yake 39% ziliishia kwenye kutolewa. Kukabiliana na mahitaji yasiyokidhiwa ya uzazi wa mpango kutapunguza kiwango cha mimba zisizotarajiwa na hivyo kupunguza uhitaji wa kutoa mimba na vifo na majeruhi ambayo kwa mara nyingi hutokea baada ya taratibu zisizo salama.”
Watafiti wamependekeza kuimarisha juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa huduma baada ya kuharibika kwa mimba, ambayo kwa sasa inapatikana bila ulinganifu katika maeneo mbalimbali. Wamependekeza uwekezaji katika kufanya huduma baada ya kuharibika kwa mimba inapatikana katika ngazi zote za mfumo wa afya, ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo watoa huduma wa ngazi ya kati na kusambaza kikamilifu dawa na vifaa vyote muhimu kwenye vituo vya afya. Pia, walisisitiza umuhimu wa kujumuisha utoaji wa huduma za uzazi wa mpango kama sehemu ya huduma baada ya kuharibika kwa mimba na kuhimiza kwamba kila mwanamke anayetibiwa kutokana na matatizo yanayohusiana na kutoka kwa mimba apewe ushauri wa kina na nyenzo za uzazi wa mpango. Hatimaye, walipendekeza kwamba utata katika sheria ya utoaji mimba ya Tanzania ufafanuliwe kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kupata utaratibu salama na wa kisheria kwa kiasi kamili kinachoruhusiwa. Watafiti wanatumaini kwamba matokeo ya utafiti huu yatasaidia kuleta mwanga kwenye sera na mipango ambayo italeta huduma za kifanisi zaidi na hatimaye kuboresha hali ya afya ya uzazi ya wanawake wote wa Tanzania.
“Matukio ya Utoaji Mimba na Huduma Baada ya Kuharibika kwa Mimba Nchini Tanzania” na Sarah C. Keogh wa Taasisi ya Guttmacher et al. inapatikana mtandaoni kupitia PLoSONE.
Utafiti huu uliweza kufanyika kutokana na misaada kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza, na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akishuhudia mabati yaliyotolewa ma Mfuko wa Pensheni LAPF kwa ajili ya ujenzi wa madarasa wilayani Geita ikiwa jitihada za Mfuko wa LAPF kuunga mkono jitihada za Serikali kutoa elimu bure. Jumla ya mabati 300 yenye thamani ya Shs. 7,000,000/= yalikabidhiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akikagua mabati yaliyokabidhiwa kama msaada na mfuko wa Pensheni wa LAPF wilayani Geita, kulia ni Meneja Masoko wa Mfuko wa LAPF Bw. James Mlowe wengine ni maofisa kutoka wilaya ya Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Mstaafu Ezekiel Kyungu akiteta jambo na Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni LAPF pamoja na mbalimbali wa Wilaya ya Geita mara baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa neno la shikrani kwa Mfuko wa Pensheni LAPF kwa msaada wa mabati 300 yanayotosheleza kuezeka vyumba sita (6) vya madarasa yanayoweza kuchukua wanafunzi 45 kwa kila chumba na hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa mazingira bora ya kufundishia.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza mmoja wa abiria anayetumia usafiri wa reli ya kati mkoani Kigoma. Kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Saveli Maketta.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mkoani Kigoma.
Muonekano wa mabehewa ya treni yakiwa mwisho wa reli ya kati, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kapteni wa Meli ya MV Liemba ya namna inavyoendeshwa, mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akipata ufafanuzi wa namna ya injini za Meli ya MV Liemba zinavyofanya kazi wakati alipotembelea Meli hiyo mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye kizibao cha njano), akimsikiliza Kapteni Winton Mwassa (wa kwanza kulia), kutoka Kampuni ya huduma za meli mkoani Kigoma mara baada ya kutembelea na kuona hali ya MV Liemba.
……………………………………………………………………
Serikali imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi-Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.
“Kama Serikali tumewekeza vya kutosha katika TRL, hivyo tunawataka mfanye biashara itakayolipa nasi tutahakikisha popote reli ilipo inatoa huduma iliyokusudiwa na kuchangia kukuza uchumi wa nchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TRL kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kupata bidhaa na abiria wengi wa kuwasafirisha nchini kote.
Amesema Serikali imedhamiria kuliongezea nguvu TRL ambapo baadhi ya mitambo kutoka Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) itakabidhiwa kwa shirika hilo hivyo kulitaka kuwa na mpango madhubuti wa kufanya biashara na kurudisha hadhi ya usafiri wa reli hapa nchini.
“Fanyeni bidii ili mpate mzigo wa kusafirisha kutoka Tanga kwenda Moshi na Arusha ili kufikia lengo la kubeba mzigo wa tani milioni moja kwa mwaka”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Amezungumzia umuhimu wa TRL kuafanya kazi kwa karibu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), ili kuongeza kasi ya huduma za uchukuzi nchini, kuongeza fursa za ajira na kukuza pato la shirika na taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Bw. Masanja Kadogosa amesema TRL imejipanga kutafuta masoko ndani na nje ya nchi ili kuboresha huduma za uchukuzi na kukuza pato lake.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua Meli ya MV Liemba na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuhakikisha meli za MV Liemba na MV Mwongozo zinakaguliwa na kufanya kazi inavyostahili katika Ziwa la Tanganyika.
“Tumieni fursa ya kuwa karibu na nchi za maziwa makuu kufanya biashara ili meli zetu zipate mzigo wa kutosha na kuongeza mapato kwa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa ambaye yupo katika ziara mkoani Kigoma amewataka viongozi na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuibua fursa za kiuchumi katika ukanda wa magharibi na hivyo kufufua miundombinu itakayochochea uchumi wa mikoa ya magharibi mwa Tanzania yenye fursa nyingi za kibiashara.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano