Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa mambo ya kale na wafanyakazi wa mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya makabidhiano ya vituo vya Laitole na Oldupai kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Bw John Kimaro (kushoto) akikabidhi hati ya makabidhiano ya kuvikabidhi vituo vya Oldupai na Laitole kwa Mhifadhi wa Ngorongoro Dkt Freddy Manongi kwa ajili ya kuvisimamia na kuviendeleza. Katikati ni Meneja wa Idara ya Uhusiano Bw Adam Akyoo.
Kaimu mkurugenzi wa Idara ya mambo ya kale Bw John Kimaro, kwa niaba ya Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii akisaini hati ya kuvikabidhi vituo vya Oldupai na Laitole kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuvisimamia na kuviendeleza. Sherehe hizi zilifanyika katika umbi wa Ngorongoro hivi karibuni.